Muhtasari wa shughuli zetu kwa Kiswahili

Ufuatao ni muhtasari wa shughuli zetu kwa kutumia lugha ya Kiswahili

ambapo zitaambatanishwa nukuu kadhaa kuhusiana na kazi mbalimbali

tulizowahi kuzifanya.

Shemweta.com
© 2021 Shemweta.com
Alfred Shemweta, (pichani juu), asili yake ni  Tanzania. Pamoja na mambo mengine Shemweta ana uzoeufu wa miaka mingi katika Taaluma ya Ukalimani, ni Mchua Misuli Kitaalamu Michezoni, Mtunzi wa Vitabu na Makala na ni Mshauri katika Stadi za Michezo-, Afya- na Elimu. Hali kadhalika Shemweta ni Mwanariadha mstaafu wa mbio ndefu na anayeheshimika nchini Sweden ambapo moja ya mafanikio yake ni ubingwa kwa miaka miwili mfululizo ( 1999 na 2000 ) katika Stockholm Marathon. Baadhi ya kazi zake zimesajiliwa katika Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA).

Nukuu mbalimbali

1. “Tumeridhishwa sana na mchango wa Alfred (Shemweta) ambapo amekuwa akionyesha moyo wa kujituma na kila mara akiwa na mtazamo chanya na hatimaye kupelekea mafanikio. Vivyo hivyo Alfred ni msimamizi mzuri na tunatumaini kutumia maarifa yake mara nyingi zaidi”. - Mkurugenzi wa Elimu, Taasisi ya Masomo na Elimu ya Michezo (SISU Idrottsutbildarna) Stockholm- Sweden, Tarehe 5/10/2003. 2. “Tuzo hii ya Heshima hutolewa kwa watu ambao kutokana na shughuli zao huchangia kuitangaza Manispaa yetu, wakifanya kazi kwa malengo thabiti na matumaini mema kwa siku za usoni na vilevile wakiwa mfano bora kwa kizazi kijacho hapa Huddinge”. - Manispaa ya Huddinge (Sweden) ikishirikiana na Jumuiya ya Makampuni Huddinge (Tuzo ya Dhahabu Mwaka 2000 - Michezo). 3. “…Zipo sura (za kitabu Miongozo Yakinifu Sekta ya Michezo) zinazoonyesha bayana zitaweza kutoa mchango mzuri sana kwa viongozi na walimu katika medani hii. Ni vizuri wahusika katika sekta hii wakakisoma kitabu hiki”. - Maoni: Taasisi ya Elimu Tanzania (Baada ya uhakiki wa kitabu tajwa), Tarehe 22/8/2011.

Historia, shughuli, bidhaa na changamoto 

Shemweta.com ni tovuti kwa ajili ya kuufahamisha umma juu ya shughuli mbalimbali za Alfred Shemweta kama vile utoaji wa ushauri wa kitaalamu katika Sekta za Michezo, Elimu, Afya, Utamaduni na Maendeleo kwa ujumla. Shughuli hizi zilikuwa zikiendeshwa chini ya Shemweta Invest AB (SIAB)  ambayo sasa imekoma. Walengwa wa shughuli na bidhaa zetu ni shule za msingi na sekondari, vyuo na taasisi mbalimbali za elimu, vyama- vilabu na jumuiya za michezo, kampuni binafsi na kampuni za umma na pia taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali. Njia tutumiazo katika utekelezaji wa kazi, shughuli na majukumu mbalimbali ni pamoja na semina za kielimu au kozi fupi-fupi, matukio ya michezo na kwa kupitia vitabu mbalimbali vya Elimu ya Michezo. Hali kadhalika uhamasishaji kuhusu maendeleo ya Michezo, Afya, Utamaduni kwa kupitia vyombo vya habari (uandishi wa makala katika Magazeti, vipindi vya Televisheni, picha za video, n.k) nayo ni njia tutumiayo katika kazi zetu. Vivyohivyo, huduma za Kukanda/Kusinga misuli kitaalamu hususan kwa wanamichezo, Tiba Mazoezi na Huduma za Utengemao nazo hujumuishwa katika kazi zetu. Mbali na Sekta tajwa hapo juu, Kampuni hii ina uzoefu wa miaka mingi katika utoaji wa huduma za ukalimani na kutafsiri nyaraka mbalimbali zikiwemo za kisheria. Wateja wakuu wa huduma hii ni pamoja na Mamlaka mbalimbali za dola na zile za Sheria na Mahakama. Lengo letu kuu ni kuimarisha shughuli za kibiashara nchini Sweden na pia kufanya kazi na washirika waliyo nje ya Sweden - hususan nchini Tanzania. Washirika wetu kibiashara kwa upande wa Tanzania ni RESTORATIVE  & REHABILITATIVE CENTRE iliyopo Dar Es Salaam. Pamoja na changamoto mbalimbali katika miaka iliyopita, Restorative & Rehabilitative Centre ndiyo itakayokuwa daraja pekee la kuunganisha washirika wetu wa Sweden na wale wa Tanzania. Wafuatao ni baadhi ya wateja/washirika (wa zamani na wa sasa) walioridhishwa na utendaji kazi wetu: Africana Travel (sasa African Tours & Safaris), Urban Tribes, Friskis & Svettis Riks, Sport-Expressen TV, Springtime Travel AB, adidas Sverige AB, Runners Store i Sverige AB, Svensk Idrotts Studie- och Utbildningsorganisation (SISU, Stockholm), Electrolux AB- Stockholm, Stockholm Marathon/Tjejmilen AB, SVT’s Intresseförening, Rotary Club Järfälla, UNICEF-Sweden, pamoja na Kampuni zilizopasishwa kutafuta wakalimani na wafasiri kama vile Semantix, Botkyrka Tolkförmedling, Språkservice Sverige AB na Järva Tolk och Översättning AB. Kwa upande wa Tanzania, SIAB iliweza (kwa mafanikio makubwa) kuandaa Semina ya siku moja huko Zanzibar kuhusu Uongozi Michezoni. Hali kadhalika tuliweza kuandaa, kwa mafanikio makubwa vilevile, matukio ya michezo yaliyokubalika vyema. Kwa upande wa Tanzania  Bara tulifanikiwa kuandaa mashindano ya riadha yaliyojulikana kama Dar Es Salaam International Athletics Meeting (DIAM – Road Race) na kwa upande wa Tanzania visiwani Zanzibar International Athletics Meeting (ZIAM – Road Race). Tunaendelea kuviwekea mazingira bora vitabu vya Alfred Shemweta pamoja maandiko mengine katika uwanda wa somo la Elimu ya Michezo (Physical Education) na stadi nyingine zinazogusa uwanda huo wa kazi nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. KARIBUNI SANA!
See us as a resource!
Muhtasari wa shughuli zetu kwa Kiswahili

Ufuatao ni muhtasari wa shughuli zetu kwa

kutumia lugha ya Kiswahili ambapo

zitaambatanishwa nukuu kadhaa kuhusiana

na kazi mbalimbali tulizowahi kuzifanya.

Shemweta.com
© 2021 Shemweta.com
Alfred Shemweta, (pichani juu), asili yake ni  Tanzania. Pamoja na mambo mengine Shemweta ana uzoeufu wa miaka mingi katika Taaluma ya Ukalimani, ni Mchua Misuli Kitaalamu Michezoni, Mtunzi wa Vitabu na Makala na ni Mshauri katika Stadi za Michezo-, Afya- na Elimu. Hali kadhalika Shemweta ni Mwanariadha mstaafu wa mbio ndefu na anayeheshimika nchini Sweden ambapo moja ya mafanikio yake ni ubingwa kwa miaka miwili mfululizo ( 1999 na 2000 ) katika Stockholm Marathon. Baadhi ya kazi zake zimesajiliwa katika Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA).

Nukuu mbalimbali

1. “Tumeridhishwa sana na mchango wa Alfred (Shemweta) ambapo amekuwa akionyesha moyo wa kujituma na kila mara akiwa na mtazamo chanya na hatimaye kupelekea mafanikio. Vivyo hivyo Alfred ni msimamizi mzuri na tunatumaini kutumia maarifa yake mara nyingi zaidi”. - Mkurugenzi wa Elimu, Taasisi ya Masomo na Elimu ya Michezo (SISU Idrottsutbildarna) Stockholm-Sweden, Tarehe 5/10/2003. 2. “Tuzo hii ya Heshima hutolewa kwa watu ambao kutokana na shughuli zao huchangia kuitangaza Manispaa yetu, wakifanya kazi kwa malengo thabiti na matumaini mema kwa siku za usoni na vilevile wakiwa mfano bora kwa kizazi kijacho hapa Huddinge”. - Manispaa ya Huddinge (Sweden) ikishirikiana na Jumuiya ya Makampuni Huddinge (Tuzo ya Dhahabu Mwaka 2000 - Michezo). 3. “…Zipo sura (za kitabu Miongozo Yakinifu Sekta ya Michezo) zinazoonyesha bayana zitaweza kutoa mchango mzuri sana kwa viongozi na walimu katika medani hii. Ni vizuri wahusika katika sekta hii wakakisoma kitabu hiki”. - Maoni: Taasisi ya Elimu Tanzania (Baada ya uhakiki wa kitabu tajwa), Tarehe 22/8/2011.

Historia, shughuli, bidhaa na changamoto 

Shemweta.com ni tovuti kwa ajili ya kuufahamisha umma juu ya shughuli mbalimbali za Alfred Shemweta kama vile utoaji wa ushauri wa kitaalamu katika Sekta za Michezo, Elimu, Afya, Utamaduni na Maendeleo kwa ujumla. Shughuli hizi zilikuwa zikiendeshwa chini ya Shemweta Invest AB (SIAB) ambayo sasa imekoma. Walengwa wa shughuli na bidhaa zetu ni shule za msingi na sekondari, vyuo na taasisi mbalimbali za elimu, vyama- vilabu na jumuiya za michezo, kampuni binafsi na kampuni za umma na pia taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali. Njia tutumiazo katika utekelezaji wa kazi, shughuli na majukumu mbalimbali ni pamoja na semina za kielimu au kozi fupi-fupi, matukio ya michezo na kwa kupitia vitabu mbalimbali vya Elimu ya Michezo. Hali kadhalika uhamasishaji kuhusu maendeleo ya Michezo, Afya, Utamaduni kwa kupitia vyombo vya habari (uandishi wa makala katika Magazeti, vipindi vya Televisheni, picha za video, n.k) nayo ni njia tutumiayo katika kazi zetu. Vivyohivyo, huduma za Kukanda/Kusinga misuli kitaalamu hususan kwa wanamichezo, Tiba Mazoezi na Huduma za Utengemao nazo hujumuishwa katika kazi zetu. Mbali na Sekta tajwa hapo juu, Kampuni hii ina uzoefu wa miaka mingi katika utoaji wa huduma za ukalimani na kutafsiri nyaraka mbalimbali zikiwemo za kisheria. Wateja wakuu wa huduma hii ni pamoja na Mamlaka mbalimbali za dola na zile za Sheria na Mahakama. Lengo letu kuu ni kuimarisha shughuli za kibiashara nchini Sweden na pia kufanya kazi na washirika waliyo nje ya Sweden - hususan nchini Tanzania. Washirika wetu kibiashara kwa upande wa Tanzania ni RESTORATIVE  & REHABILITATIVE CENTRE iliyopo Dar Es Salaam. Pamoja na changamoto mbalimbali katika miaka iliyopita, Restorative & Rehabilitative Centre ndiyo itakayokuwa daraja pekee la kuunganisha washirika wetu wa Sweden na wale wa Tanzania. Wafuatao ni baadhi ya wateja/washirika (wa zamani na wa sasa) walioridhishwa na utendaji kazi wetu: Africana Travel (sasa African Tours & Safaris), Urban Tribes, Friskis & Svettis Riks, Sport- Expressen TV, Springtime Travel AB, adidas Sverige AB, Runners Store i Sverige AB, Svensk Idrotts Studie- och Utbildningsorganisation (SISU, Stockholm), Electrolux AB- Stockholm, Stockholm Marathon/Tjejmilen AB, SVT’s Intresseförening, Rotary Club Järfälla, UNICEF- Sweden, pamoja na Kampuni zilizopasishwa kutafuta wakalimani na wafasiri kama vile Semantix, Botkyrka Tolkförmedling, Språkservice Sverige AB na Järva Tolk och Översättning AB. Kwa upande wa Tanzania, SIAB iliweza (kwa mafanikio makubwa) kuandaa Semina ya siku moja huko Zanzibar kuhusu Uongozi Michezoni. Hali kadhalika tuliweza kuandaa, kwa mafanikio makubwa vilevile, matukio ya michezo yaliyokubalika vyema. Kwa upande wa Tanzania  Bara tulifanikiwa kuandaa mashindano ya riadha yaliyojulikana kama Dar Es Salaam International Athletics Meeting (DIAM – Road Race) na kwa upande wa Tanzania visiwani Zanzibar International Athletics Meeting (ZIAM – Road Race). Tunaendelea kuviwekea mazingira bora vitabu vya Alfred Shemweta pamoja maandiko mengine katika uwanda wa somo la Elimu ya Michezo (Physical Education) na stadi nyingine zinazogusa uwanda huo wa kazi nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. KARIBUNI SANA!
See us as a resource!